Mitundu Yetu
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.


chat with friends
 
HomePortalGalleryLatest imagesSearchRegisterLog in

 

 The darkness planet 01

Go down 
AuthorMessage
Princes




Posts : 3
Join date : 2016-10-14

The darkness planet 01 Empty
PostSubject: The darkness planet 01   The darkness planet 01 Icon_minitimeSat Oct 15, 2016 6:57 am

EMMANUEL Muhuge Magende, mkazi wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam anasimulia kisa alichowahi kukumbana nacho miaka mitatu (2010) nyuma baada ya kugongwa na gari dogo akiwa

anavuka barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni, jirani na msikiti.
Anasema: Nakumbuka ilikuwa tarehe kumi na tisa, mwezi wa saba, nilipanda daladala pale sokoni

Kariakoo. Hili daladala lilikuwa likienda Mwenge kupitia Kinondoni kisha kupita Morocco na kuunga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Nilikaa kwenye siti ya kwanza mlangoni. Wakati naingia, kwenye siti hiyo alikaa mzee mmoja kwa makadirio ya umri alikuwa kama ana miaka sabini hivi.
Huyu mzee mimi nilipoingia tu, akasimama na kuniambia nikae pale ambapo pembeni yake palikuwa na abiria. Nilimkatalia kwa sababu daladala lenyewe lilijaa, sasa mzee kama yeye akiniachia siti mimi ambaye wakati huo nilikuwa na miaka 45 nilihisi si sawa.
Cha ajabu huyu mzee alilazimisha sana akisema yeye anakwenda kukaa siti ya nyuma. Ilifika mahali nilimkubalia, nikakaa yeye akatoka kuelekea nyuma lakini sikumfuatilia hadi kukaa kwake.
Muda huohuo, daladala liliondoka, likapita njia yake hadi Faya ambapo halikusimama kwa sababu nafasi haikuwepo. Kufika Magomeni ya Hospitali, daladala lilisimama, abiria walishuka wengi tu hadi nafasi ya kukaa watu wengine ikabaki. Wakati abiria wakishuka nilikuwa namwangalia mmoja baada ya mwingine ili kama kuna yule mzee nimwambie namlipia nauli, lakini hakuwepo, nikajua bado yupo ndani.
Daladala lilipoondoka hapo halikusimama Kituo cha Morocco Hotel mpaka Mkwajuni ambapo mimi nilikuwa nashuka. Kwa kuwa nilikuwa jirani na kondakta nilimwambia shusha hapo Mkwajuni, akagonga daladala likasimama. Nilisimama huku nikimwangalia yule mzee ili nimwambie namlipia, lakini sikumwona!
Nilishuka, kufika chini nikasimama ili kuvuka barabara maana nilikuwa naishi upande wa pili wa kituo hicho.
Cha ajabu sana nikamwona yule mzee kwa ng’ambo akiwa anatembea kwenda uelekeo uleule ninaokwenda mimi.
Nilivuka barabara haraka ili nimuwahi, lakini nikiwa katikati ya barabara hiyo gari dogo, jekundu, lilitokea upande wa Kinondoni Studio na kunifuata kwa kasi. Nilifanya jitihada zote kulikwepa lakini ilishindikana, likanigonga! Sikujua kilichoendelea.
***
Mbele yangu kulikuwa na jumba kubwa la kifahari, sikujua kama wanaishi wanadamu au la! Nilitembea kuelekea kwenye ile nyumba. Ilijengwa si kwa matofali wala simenti, ilionekana kama vioo vya kujitazamia ndivyo vilitumika sana.
Nilikuwa katika hali ya kuogopa sana, hivyo kufika kwangu kwenye nyumba ile kulikuwa na maana ya kuomba msaada. Kuogopa kulisababishwa na mazingira, sikuona jua, sikuona mawingu wala sikuona ardhi, nilitembea juu ya vioo.
Ili uingie mlangoni kulikuwa na ngazi tatu. Nilikanyaga ya kwanza na ya pili, nilipotaka kukanyaga ya tatu, mlango ulifunguka wenyewe nikaingia kama kwa kulazimishwa.
Ndani niliwakuta watu wengi weupe, naweza kusema walikuwa Wazungu pia naweza kusema walikuwa Waarabu, lakini hakukuwa na mtu mweusi hata mmoja.
Watu wote waliniangalia nilipokuwa naingia, wakanishangilia sana huku wengine wakiwa wanapiga vigelegele. Lakini pamoja na vigelegele hakukuwa na mwanamke.
Walikuwa wanaume wenye midevu mingi, warefu mfano wa watu warefu wakiwa wawili kwa kwenda juu hivyo mimi nilikuwa nawaangalia kwa juu.
Mmoja alinifuata na kunishika mkono. Akatembea na mimi hadi kwa wenzake, mmoja akanipokea hapo akanipeleka mbele ya jumba hilo ambako pia kulikuwa na mlango mkubwa kama niliouingia.
“Unajua uko wapi hapa?” aliniuliza.
“Niko ugenini.”
“Ni ugenini ndiyo, ni wapi?”
“Mimi sijui.”
“Ngoja nikuoneshe ulikotoka,” alisema yule mtu na kunitoa nje, tulitoka na yeye, akanyoosha mkono kuangalia juu huku akisema:
“Unakuona kule?”
Niliinua macho na kuangalia juu, nikaona dude kubwa likiwaka kama mwanga wa taa za kisasa.
“Umeona kule?” yule mtu aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Ni nini?”
“Dude.”
“Siyo dude, wewe umetoka kule.”
“Ina maana ile ni dunia?”
“Ile ni dunia, na pembeni yake unachokiona kidogo ni mwezi.”
“Huku sasa ni wapi?”
“Huku sasa ndiko wanakokuja watu waliokufa wakisubiri kupewa adhabu.”
“Ina maana mimi nimekufa?” nilimuuliza, akacheka sana kuonesha kwamba mimi ni mjinga sana kama sijui kama nimekufa.
“Unataka kujua kama umekufa au la!”
“Ndiyo, nataka kujua.”
Alinirudisha ndani ambapo hakukuwa na mtu hata mmoja, tukatembea kuelekea upande wa mashariki mwa jumba hilo hadi kwenye mlango mwingine mkubwa sana, ukafunguka wenyewe. Tuliingia ndani ambako tulikuta watu mchanganyiko, wengine weusi kama mimi wengine weupe.
Walikuwa wamekaa wakiangalia skrini moja kubwa sana. Ndani ya skrini hiyo kulikuwa na watu wanafanya mambo mbalimbali. Wengine walikuwa wanafanya zinaa, wengine wanaiba, wengine wanapigana, wengine wanachinja binadamu wenzao.
Kifupi ni kwamba watu walikuwa wakifanya madhambi ndicho nilichokibaini mimi.
Watu wote walikuwa wamekodolea macho ile skrini, lakini tulipoingia sisi wakageuka kutuangalia. Mmoja akauliza:
“Huyo naye haamini kama amekufa?”
Yule niliyekuwa naye akajibu:
“Ndiyo.”
Nilikaribishwa kiti nikakaa halafu skrini ikazimwa. Baada ya muda ikaanza kuonesha picha yangu. Nilionekana napanda daladala Kariakoo. Picha hiyo ikanionesha nikiwa nazungumza na yule mzee akisema anipishe kwenye kiti chake.
Cha ajabu, huyo mzee awali alionekana kama nilivyomwona mimi lakini ghafla akageuka, akawa mweupe kama watu niliowakuta kwenye lile jumba.
Tukio zima lilionekana, daladala likipita Magomeni, likakata kona kwenda Hospitali na kupita Hoteli ya Morocco hadi Mkwajuni.
Nilimwona yule mzee akitoka kwenye daladala kwa kupitia kioo cha mbele cha dereva kisha akavuka barabara kabla hata daladala halijasimama.
Nilionekana nashuka, natembea kwenda kuvuka barabara. Lile gari jekundu lilizuka tu palepale jirani yangu na kunigonga.

Je, kiliendelea nini? Tuonane jioni ...
Back to top Go down
 
The darkness planet 01
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Mitundu Yetu :: aminmas :: Your first forum-
Jump to: